Friday , 22nd Jan , 2016

Baada ya kutangazwa kwa kamati 18 za kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari kamati nyingi zimefanya uchaguzi wa wenyeviti na makamu wao huku Chama cha Mapinduzi kikiongoza kwa kamati karibu zote.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) anatakiwa kutoka upinzani hivyo bado hajachaguliwa ila makamu wake aliyechaguliwa ni mbunge wa Sumbawanga Mjini Aeshi K. Hilary (CCM).

Na kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mwenyekiti atatoka upinzani na hajafahamika Makamu ni mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM).

Waliochaguliwa katika kamati nyingine ni pamoja na mbunge wa Kigoma Kaskazini Peter Serukamba (CCM) ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, na Makamu wa wake ni Mbunge wa Busega Raphaeli Chegeni (CCM).

Kamati ya Sheria ndogo itaongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge (CCM) na makamu wake ni mbunge wa Sengerema William Ngeleja (CCM)

Kamati ya Nishati na Madini mwenyekiti ni mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Singida Martha Mlata na makamu wake ni mbunge jimbo la Chumbuni Ussi Pondeza (CCM).

Soma zaidi majina hapa kwenye PDF