Monday , 7th Nov , 2016

Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, John Mallya, amesema chama hicho kimefungua kesi Mahakama Kuu kutaka Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema, afikishwe Mahakamani baada ya kukaa Mahabusu kwa muda wa siku 6 kinyume cha sheria.

Godbless Lema - Mbunge wa Arusha Mjini

Wakili Mallya amedai kwamba, mtuhumiwa anapaswa kukaa ndani kwa saa 24 tu kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai hivyo kesi waliyofungua imedhamiria kuwataka RCO, Mwenasheria Mkuu na IGP wamlete Mh. Lema Mahakamani kwa amri ya Mahakama.

Hata hivyo kwa upande wake, Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limesema, upelelezi kuhusu mbunge huyo wa bado haujakamilika.

Wiki iliyopita, Mh. Lema alisafirishwa kutoka Bungeni mjini Dodoma hadi Arusha na kuswekwa rumande kwa kile kichoelezwa na Kamanda wa Polisi Arusha, Charles Mkumbo, kutoa maneno ya uchochezi na kuyarudiarudia.

John Mallya - Wakili wa CHADEMA