Thursday , 20th Oct , 2016

Chama cha Wananchi CUF kimefungua kesi dhidi ya msajili wa vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na msajili huyo, Prof. Ibrahim Lipumba.

Jaji Francis Mutungi

 

Kesi hiyo namba 23 ya mwaka 2016 ilifinguliwa baada ya mahakama kuu, kanda ya Dar es salaam kuridhia maombi ya chama hicho ya kumfunguliwa kesi msajili.

Wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali AG na wananchi 11 waliosimamishwa uanachana na CUF, akiwamo Naibu Katibu Mkuu Bara amabye pia ni Mbunge wa Kaliua Magdalena Sakaya.

Maombi mengine katika kesi hiyo ni Mahakama itoe amri kubatilisha barua ya msajili inayomtambua Prof. Lipumba kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho.

Bodi hiyo pia imeomba Mahakama itoe amri ya kumzuia Msajili kufanya kazi nje ya mipaka ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yake na kumuia kuingilia masuala ya kiutalawa ndani ya chama hicho.