
Baadhi ya barabara za jiji la Dar es Salaam zitakavyokuwa pindi mradi wa mabasi yaendayo haraka wa DART utakavyokamilika.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Meneja wa Matumizi ya barabara wa DART , Mhandisi Mohamed Kuganda wakati akielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zilizopo katika utekelezaji wa mradi huo katika awamu ya kwanza.
Aidha, Mhandisi Kuganda ameelezea kasi ya mradi huo kuathirika kutokana na wafanyakazi wa kampuni ya STRABAG iliyopewa dhamana ya ujenzi katika mradi huo kugoma mara kwa mara hali inayoathiri kukamilika kwa mradi huo kwa wakati pamoja na changamoto nyingine zinazo zorotesha mradi.