
Farid Musa
Awali wasiwasi ulikuwa umetanda kwamba huenda ndoto za Farid kucheza soka la kulipwa Ulaya zikawa zimefifia kutokana na baadhi ya vibali kushindwa kukamilika kama ilivyotarajiwa.
Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed amethibitisha kukamilika kwa kibali ambacho kitamruhusu Farid kufanya kazi nchini Hispania na ameahidi kuwa, klabu inafanya jitihada kuhakikisha Farid anaondoka mapema kwenda kujiunga na klabu yake ya Tenerife.
“Kibali chake cha kazi kimetoka siku moja ama mbili zilizopita, sasa hivi tunasubiri kukamilika kwa baadhi ya taratibu na punde Farid ataelekea nchini Hispania kwenye timu ya Tenerife kwa ajili ya kuanza maisha yake mapya,” amethibitisha Abdul Mohamed.
“ITC ya Farid imetumwa muda mrefu sana ipo Tenerife masuala ya ITC na makubaliano kati ya klabu na klabu tulishamaliza kilichokuwa kinasubiriwa ni kibali cha kazi kutoka ili kwenda kufanya kazi.”
“Tunaamini punde Farid ataanza safari yake, tunajitahidi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu kila jambo liwe limekamilika.”