Thursday , 5th Jun , 2014

Wakazi kutoka zaidi ya kaya 4,000 katika eneo la Chasimba kata ya Bunju manispaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam, bado hawajui hatma ya makazi yao, licha ya serikali kuingilia kati mgogoro kati ya kiwanda cha saruji cha Wazo Hill na wananchi hao.

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka. Wizara yake ina ndiyo inayoshughulikia suala la fidia kwa wakazi wa Chasimba.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Basihaya Bw. Daniel Aron amesema kuwa mgogoro huo umetimiza miaka miwili sasa tangu serikali iahidi kushughulikia tatizo hilo, na kwamba kwa muda wote huo hawajaonyeshwa eneo watakalohamishiwa licha ya kuambiwa eneo hilo lipo tayari.

Bw.Aron amesema serikali iliahidi kuwapa maeneo au fidia ambapo mpaka sasa wakazi 3,060 wameshafungua akaunti katika benki mbalimbali ili kuwekewa fedha za fidia pasipo mafanikio.