
Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwasa
Matembezi hayo yaliyopokelewa na mkuu wa mkoa wa Geita Bi Fatma Mwasa yamelenga kuhakikisha ukatili wa mauaji ya kinyama unakomeshwa katika mkoa wa Geita ili kuifanya Geita kuwa sehemu salama ya kuishi.
Pamoja na matembezi hayo kuungwa mkono na kada mbalimbali za kiserikali na watu binafsi jamii imewalalamikia wabunge wa mkoa wa Geita kutoshiriki matukio makubwa yanayotokea katika majimbo yao, hasa tukio la kuibiwa hatimaye kuuwawa kwa mtoto Yohana Bahati, hali ambayo inaashiria kuwavunja moyo wananchi kuwa wabunge wao si wanajamii wenzao.
Waganga wa jadi pia wamejitokeza kuungana na jamii kulaani mauaji hayo na kuomba kibali kwa uongozi wa mkoa wawaruhusu kuendesha msako wa kuwabaini waganga wenye kufanya uganga unaosababisha madhara kwa jamii.