Thursday , 13th Oct , 2016

Harakati za miezi sita za kumsaka mrithi wa Katibu Mkuu wa sasa wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, zimefikia ukingoni leo baada ya Baraza Kuu la Umoja huo kupitisha uteuzi wa Antonio Guterres kuwa Katibu Mkuu mpya .

Antonio Guterres

Bw. Guterres alipendekezwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumrithi Ban Ki Moon

Akizungumza mara baada ya kuidhinishwa, Bw. Guterres ameshukuru jinsi mchakato wa kumpata Katibu Mkuu mpya ulivyokuwa wa wazi na uliotoa washindani mbalimbali wenye uwezo.

Ameahidi kutumikia nchi zote kwa usawa bila bila upendeleo

Antonio Guterres amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Ureno na pia amehudumu kama Kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kwa miaka kumi na anatarajiwa kuanza kuitumia nafasi hiyo Novemba Mosi mwakahuu, baada ya Ban Ki-moon kumaliza muda wake Oktoba 31.