Thursday , 5th Jun , 2014

Wanafunzi wa taasisi ya Teknolojia (DIT) ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wameruhusiwa kufanya mitihani baada ya mgomo wao uliodumu kwa siku mbili mfululizo.

Waziri wa sayansi na teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.

Mgomo huo uliopelekea baadhi yao kuandamana hadi wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kupinga wanafunzi wenzao kutoruhusiwa kufanya mitihani kutokana na kutokamilisha malipo ya ada.

Akizungumza na East Africa Radio rais wa taasisi hiyo Himida Elihuruma amesema kuwa Katibu mkuu wa wizara hiyo Patrick Makungu aliutaka uongozi wa chuo kuwaruhusu wanafunzi kufanya mitihani yao kwa sharti la kuzuiwa matokeo yao mpaka watakapolipa ada wanayodaiwa.

Kwa upande wake Afisa uhusiano wa taasisi hiyo Amani Kakana amesema uongozi umekaa kikao na kujadili agizo la wizara na kuwa ratiba ya mitihani itatoka baada ya kikao hicho.