
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi la Umeme nchini (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi la kuwakatia umeme wadaiwa wa shirika hilo Mwenyekiti wa kamati inayokagua miundombinu ya umeme John Manyama amesema zoezi hilo limeshafanyika katika mikoa 17 nchini.
Mhandisi Manyama amesema kuwa mpaka sasa katika opereshini hiyo wamebaini zaidi ya hasara ya shilingi bilioni 1 kutokana na uharibifu na wizi wa miundombinu ya umeme nchini.
Mpaka sasa TANESCO, imeshakagua wateja 3800 smbapo wateja 180 wamebainika kuwa na matatizo mbalimbali yanayohusiana na wizi wa umeme katika jiji la Dar es Salaam pekee.