
Watoto wenye ulemavu na mtindio wa ubongo wakiwa katika moja ya maadhimisho (Picha na Maktaba|)
Pia serikali imetakiwa kuongeza jitihada katika kutatua changamoto zinazowakabili watoto hao.
Hayo yamezungumzwa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi na Watoto wenye Mtindio wa Ubongo Bw. James Nyamkole ambapo amesema kuna baadhi ya familia zinafarakanakwa sababu ya watoto wenye elemavu huku wengine wakiwaficha ndani na wengine wakilihusisha jambo hilo na imani za kishirikina.
Bw. James amesema kupitia chama cha wameamua kutoa elimu kwa jamii juu ya suala la kuwashughulikia watoto wenye mtindio wa ubongo ili kutatua changamoto zinazowakabili hao ikiwemo kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu na huduma za kiafya.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa kwa upande wa serikali nayo bado haijafanya jitihada za kutosha kuwapatia watoto hao huduma muhimu ikiwemo mazoezi tiba pamoja na miundombinu rafiki kwa ajili ya kuwapatia elimu.