Wednesday , 30th Mar , 2016

Serikali ya Tanzania na Japani zimetiliana saini hati ya makubaliano zitakazoiwezesha Tanzania k

Serikali ya Tanzania na Japani zimetiliana saini hati ya makubaliano zitakazoiwezesha Tanzania kupata mkopo wa takribani shilingi bilioni 114.6 ambazo zitatumika katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016-2017.

Akiongea mara baada ya kusaini hati hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Cervacius Likwelile, amesema kuwa mkopo huo utaelekezwa katika bajeti ya serikali ya mwaka2016-2017 ili kuboresha mazingira ya biashara hapa nchi na kupanua fursa za ajira.

Aidha, nchi hizo mbili zimefanya marekebisho ya hati ya makubaliano ya wataalamu wa kujitolea kuja nchini kutoa huduma katika sekta mbalimbali kwani hati hiyo ilisainiwa mwaka 1966 hivyo haiendani na mabadiliko yaliyopo hivi sasa ili kuwawezesha wataalam hao kuweza kuja nchini bila ya vikwazo vyovyote.

Kwa upande wake Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida amesema kuwa Serikali ya Japani ina imani kubwa na uongozi uliopo kwa hivi sasa na wanaamini kuwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili utasaidia kukuza maendeleo ya uchumi na kijamii.