Saturday , 1st Dec , 2018

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dk Bashiru Ally amemtaka kada wa chama hicho Bernard Membe kufuata taratibu zinazotumika na chama hicho kwa ajili ya kukutana.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Dk Bashiru Ally amemtaka kada wa chama hicho Bernard Membe.

Dkt Bashiru ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Disemba 1, 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Amedai katika miaka 10 iliyopita CCM haikufanya vizuri kutokana kikundi cha wachache kujifanya ndiyo wenye nguvu jambo lililosababisha chama kisipendwe na wapiga kura na kuongeza  tangu achaguliwe kuwa Katibu Mkuu hajawahi kuonana na Membe na licha ya chaguzi zote zinazofanyika za kurudisha wabunge.

"Sikumsema Membe kama mtu maarufu au mwenye nguvu bali nimemsema kama mwanachama wa kawaida, hana tofauti kabisa na wanachama walioingia leo, ila ana tofauti kwa kuwa amekuwa waziri na mbunge” amesema Dkt Bashiru.

Namuhitaji sana Membe, ningekuwa na namba yake ya simu ningempigia,” ameongeza.