
James Lembeli
Mbunge wa jimbo la Kahama Mkoani Shinyanga Mhe. James Daudi Lembeli ametangaza rasmi hii leo kuachana na chama tawala CCM na kujiunga na chama cha siasa cha upinzani cha CHADEMA.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari Mhe. Lembeli amesema ameamua kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa chama cha CCM kimekiuka taratibu na Katiba yake huku viongozi wake wakikaa kimya.
Mhe. Lembeli pia ameibua tuhuma nzito za kuwepo njama za kuandaliwa majimbo bandia, utoaji wa rushwa katika mchakato wa kuwatafuta wagombea katika ngazi za udiwani na ubunge ndani ya chama cha CCM.
Mhe. Lembeli alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu katika operesheni ya kupambana na ujangili ya Tokomeza iliyopelekea kujiuzulu kwa baadhi ya mawaziri.