Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
Kishoa ametoa kauli hiyo leo Januari 14, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali kuhusu afya na maendeleo ya Lissu.
“Lissu ni kaka yangu, ni mbunge mwenzangu na kiongozi wangu, mambo ya kuangalia ni kupata baraka za chama lakini anafaa,” amesema Kishoa.
Amesema wakati ukifika atatamani kuona jina la Lissu likipitishwa kuwania urais, kwa kuwa Watanzania wanajua msimamo wa kiongozi huyo na ndio anayefaa kuwaongoza.
Lissu kwa sasa anaendelea na ziara yake kwenye nchi za Ulaya na marekani kwa ajili ya kuelezea mkasa wa kupigwa risasi uliompata Septemba 2017 Jijini Dodoma.