
Madawa ya kulevya
Kamishna Siyanga amesema hayo leo alipokutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kumhakikishia kuwa harakati za kupambana na dawa za kulevya zinaendelea vizuri, na kusema kuwa mikakati iliyowekwa itasaidia kutatua tatizo hilo na kuzuia madawa ya kulevya yasiingie nchini.
Kamishna Siyanga amesema mikakati hiyo ni pamoja na kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia madawa ya kulevya, na kutoa tiba kwa watu walioathirika na madawa ya kulevya.
Kamishna Siyanga ameendelea wa kusema kuwa tatizo la dawa la kulevya lilikuwa kubwa zaidi na kuzitaja aina ya dawa za kulevya ambazo mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroin, cocaine, kemikali bashirifu na kwamba kwa sasa wameanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi yaliyovunwa.
