Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Bi. Mndeme amesema ni vyema mikoa hiyo ikachukua tahadhari ili isijeathirika na kupata madhara makubwa kama yao, na kuleta hasara kubwa kwa jamii.
“Tunawaambia na majirani kwamba wachukue tahadhari wajikinge na ugonjwa huu, tumewaambia maafisa ugani wasikae ofisini waende 'field' kwa wakulima watoe elimu, kwa kweli ni 'disaster', kuhusu wakulima wetu tumewashauri wapande upya kwa sababu bado kuna mvua”, amesema Bi. Mndeme.
Hivi karibuni kumeripotiwa kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa mazao ya mahindi, ambapo heka 82 za wakulima wilayani Songea zimeharibiwa na wadudu.
