Monday , 5th Sep , 2016

Waandaji wa Maonesho ya Kumi ya Biashara na Bidhaa za Afrika zinazouzwa nje na zinazoingizwa ndani, wameahirisha maonesho hayo hadi tarehe za baadaye.

Muandaaji wa Maonesho ya Kumi ya Biashara na Bidhaa na Afrika zinazouzwa nje na zinazoingizwa ndani.

Maonesho hayo yameahirishwa kufuatia ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi kuwa na shughuli nyingine kwa sasa.

Muandaaji wa maonesho hayo, Solomon Kinyanjui, amesema watatangaza hivi karibuni tarehe mpya ya kufanyika maonesho hayo makubwa, ambayo katika miaka ya nyuma yamekuwa yakiwavutia watangazaji bidhaa kutoka Ulaya, Asia, Marekani na mataifa mengine ya Afrika.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa KICC, Elijah Korir alimuarifu Kinyanjui kuwa ukumbi wa Tsavo, ulishakuwa umechukuliwa mapema kwa shughuli nyingine, hivyo hautoweza kupatikana kwa maonesho hayo ya biashara yaliyopangwa kufanyika Septemba 21 na 23.