
Dkt. Charles Msonde.
Akitangaza matokeo hayo Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dkt. Charles Msonde , amesema kuwa wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa matokeo hayo baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.
"Mbali na kufuta matokeo hayo, NECTA imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani, kutokana na udanganyifu huo", amesema Dkt. Msonde
Dkt. Msonde amesema kuwa wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.