
Mbunge wa zamani Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu
Monko ametoa kauli hiyo baada ya aliyekuwa mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kumpata mgombea wa Jimbo hilo, Hussein Gulamali kushinda kesi yake ya rushwa, pamoja na tetesi za kurudi kugombea tena kwa Mbunge wa zamani Lazaro Nyalandu ambapo amedai bado hawahofii viongozi hao.
Monko ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na www.eatv.tv kwenye mahojiano maalum kufuatia siku chache Mahakama ya Mkoa wa Singida kumuachia huru kiongozi huyo ambaye alituhumiwa, kutaka kumhonga Afisa Usalama ili jina lake lipite.
"Niseme kitu kimoja nguvu ya uchaguzi ni wananchi kwa hiyo Gulamali, licha ya kuwa wa kwanza kwenye chama sio ishu kwenye chama chetu, kinachotakiwa ni uadilifu na utendaji wako, kwani alianza hapa alishaanza Dodoma na alishindwa,".
"Na wala simhofii, ana haki ya kikatiba lakini wananchi watachambua pumba na mchele nani muadilifu nani sio muadilifu." ameongeza Monko.
Kuhusu kupata upinzani kwa Mbunge wa zamani wa Jimbo hilo Monko amesema kuwa "nina msubiri kwa hamu kweli nashangaa kwanini hakurudi juzi, kuja 2020 atakuwa amechelewa wananchi watachambua uadilifu, kwa kweli hapa Singida Kaskazini ajipange labda jimbo jingine." ameongeza Monko.