
Akizungumza na www.eatv.tv Mbunge huyo wa Singida Kaskazini amesema kauli aliyoitoa hivi karibuni, ni kauli ya kisiasa bali anachojua yeye majimbo yote ya mkoa huo kwenye Uchaguzi Mkuu 2020, majimbo hayo yatabaki CCM.
"Kuhusiana na kauli ya Nyalandu sidhani kama kuna lolote, kwa sababu ni kauli ya mwanasiasa yeyote, huwezi kusema hautashinda, sasa kwa vile karudi kivingine kupitia CHADEMA lazima awaaminishe watu wanaenda kushinda japo sijajua amejipangaje kufikia mahali pa kushinda majimbo yote ya Singida, ila nachojua Mkoa wa Singida bado unapendwa sana na wananchi." amesema Justine Monko.
"Mimi nachojua majimbo yote ya Mkoa wa Singida yatabaki CCM kwa sababu kuna kazi tumezifanya, ilani ya CCM imetekelezwa kwa kiasi kikubwa, na hilo ndilo litakalotufanya tushinde." amesema Justine Monko.
Hivi karibuni akiwa mkoani Singida kwenye kampeni ya CHADEMA ni msingi Lazaro Nyalandu alisema kupitia watu maarufu wa mkoa huo akiwemo yeye pamoja na Tundu Lissu watahakikisha wanashinda majimbo yote manne ya mkoa huo.