Akisoma hukumu hiyo leo Februari 26, 2018, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dk Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuthibitisha uhusiano wa kimapenzi kati ya Dk Phills na Mchungaji Mwingira pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa ni matokeo ya uhusiano wa kimapenzi kati ya Dh Phills na Mchungaji Mwingira.
Awali katika utetezi wa Dk Phills Nyimbi, aliieleza mahakama hiyo kuwa hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.
Akiongozwa na Wakili Peter Swai kutoa ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk William Morris, Dk Nyimbi aliomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh7.5 bilioni anazodai kwa sababu hakuwa na uhusiano na Mchungaji Mwingira.
Disemba 28, 2011, Dk Morris na Dk Phills walifunga ndoa ya Kanisani na wakati wa uhusiano wao, Dk Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa kuingia katika uhusiano wa mapenzi na kubahatika kupata mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka tisa.





