Thursday , 27th Oct , 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Hellen Kijo-Bisimba ametahadharisha kuwa mikataba mbalimbali ambayo Tanzania inaingia na nchi nyingine inapaswa kuzingatia sheria ya mikataba inavyoekeza.

Daktari wa falsafa katika sheria na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dkt. Hellen Kijo-Bisimba.

 

Dkt. Kijo-Bisimba ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam ikiwa tayari Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano wa kimaendeleo na mataifa mengine na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kutumia sheria katika kuwekeana mikataba mbalimbali ya kimaendeleo baina ya nchi ili kuzuia hali ya sintofahamu kwa siku za baadaye.

Amesema mikataba mingi inayosainiwa inakuwa na migogoro siku za mbeleni kwakuwa kuna baadhi ya vipengele vinakiukwa kutokana kutokujua sheria zinavyoelekeza.

Ameongeza kuwa faida ya mikataba hiyo ni kuleta maendeleo na hasara ya mikataba isiyozingatia sheria ya mikataba ni kuibiwa mali za nchi kama ile mikataba ya madini ambayo ilikuwa inatoa mirabaha midogo kwa nchi na kama ikivunjwa nchi inalipishwa fedha nyingi.