
Matunda pamoja na mboga mboga pichani hapo juu, ni sehemu tu ya virutubisho muhimu vinavyohitajika kwa ajili ya afya na ukuaji wa watoto na akina mama wajawazito.
Kaimu mkurugenzi mtendaji kutoka Taasisi ya lishe Tanzania (TFNC), Benedict Jeje aliyasema hayo wakati wa mkutano na wadau wa lishe uliokuwa ukijadili umuhimu wa viazi lishe ambavyo ni viazi vya rangi ya chungwa au Caroti kwa watoto.
Dawa na virutubisho vinavyonunuliwa na Serikali ni pamoja na chanjo ya Vitamini A, Zink, Chuma na folic.