
Fatma Karume na Waziri Kigwangalla
Baada ya mkutano huo ambao umedumu kwa zaidi ya masaa kadhaa ukianza majira ya saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni, umemalizika kwa wawili hao kuonekana wakifurahia na kuonesha umoja tofauti na jinsi ambavyo huwa wanacharuana mitandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri Kigwangalla amesema mambo yote yamewekwa kando huku akisifu kuwa Fatma maarufu Shangazi ni mtulivu na msikivu sana.
Shangazi ni mtu poa sana, mnyenyekevu, mvumilivu, msikivu, mwenye uelewa mpana sana wa mambo, na ana sababu zake kwenye kila analofanya. Tungeweza kuongea mpaka asubuhi kwa jinsi mada zilivyokuwa nyingi, nzito na ndefu. Kwa hakika tutakutana tena. Inshaallah pic.twitter.com/sysL1qBYm5
— Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) January 13, 2019
Kwa upande wake Fatma Karume ameshukuru Kigwangalla kwa ukarimu wake pamoja na mengine ikiwemo kulipia chakula walichokula.
Hamisi and I. Thank you @HKigwangalla for a LOVELY BRUNCH. And he paid for it too! pic.twitter.com/e9XnQcycrr
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) January 13, 2019