
Waziri ameyasema hayo katika kikao cha bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kigoma mjini aliyetaka kujua lini serikali itachukua hatua za kukabiliana na ubadhirifu wa bilioni 28 za wakulima wa zao la tumbaku mkoani Tabora.
''Nimeipokea ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kwa mwaka 2013 na ninaipitia mstari hadi mstari na baada ya hapo bunge litakapomalizika nitaelekea katika chama cha ushirika mkoani Tabora kwenda kutoa jawabu ya tatizo hili''
''Napenda kusema tena kwa upande wangu hakuna uchunguzi juu ya uchunguzi (CAG) amekwisha baini ubadhirifu mimi nikienda ni kuelekeza vyombo husika kuchukua hatua za kisheria na si kuanza uchunguzi tena ''Amesisitiza Nchemba.
Aidha waziri amebainisha kuwa wizara yake imejipanga kupitia zao moja moja na masuala yote yanayohusu wakulima na kutoa ufumbuzi kwa haraka ili wananchi waweze kupata manufaa ya mazao yao.