mwenyekiti wa TACEO Martina Kabisama
Mtandao wa Asasi za kiraia zinazofuatilia Uchaguzi nchini TACEO zimeitaka Tume ya Uchaguzi nchini NEC kuhakikisha watu wote ambao hawakuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR Kuhakikisha kuwa wanaandikishwa wakati wa kuhakiki wa majina ya watu katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Hayo yametamkwa leo na mwenyekiti wa TACEO Martina Kabisama baada ya kumalizika kwa tathimini ya jinsi zoezi la uandikishaji lilivyoenda hapa nchini katiba baadhi ya mikoa na kubaini mapungufu kadhaa ikiwa ni pamoja watu wengi kutoandikishwa pamoja na baadhi ya vituo kuwa katika nyumba za ibada na kwenye zahanati, Martina ameongeza kuwa vituo vingi vya kuandikisha havikuwa na miundombinu kwa ajili ya watu wenye ulemavu, wazee na wamama wajawazito.
Aidha mtandao huo umeitaka NEC ihakikishe waandikishaji wawe na uwezo wa kutumia machine za BVR na kompyuta na kusisitiza mapungufu yote yaliyotokea mikoani yasijirudie katika mkoa wa Dar es salaam.
Kwa upande wake mkurugezi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRD Onesmo Ole Ngurumwa amelitaka jeshi la Polisi nchini kutowatisha wananchi kwa kupeleka polisi wengi katika Vituo vya kuandikisha kwani wananchi watahisi eneo hilo haliko salama.