Saturday , 26th Mar , 2016

Ofisi ya Bunge imetangaza kufanyika kwa mabadiliko ya shughuli za kamati za Bunge kuelekea mkutan

Ofisi ya Bunge imetangaza kufanyika kwa mabadiliko ya shughuli za kamati za Bunge kuelekea mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupokea mabadiliko yampango wa kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Ofisi ya Bunge imechukua uamuzi huo zikiwa zimepita wiki tatu tangu ilipotoa ratiba ya vikao vya kamati ambazo hufanyika kabla ya kuanza kwa Bunge mjini Dodoma.

Mkutano wa tatu wa Bunge ambaop utakuwa wa bajeti utaanza mwezi ujao Mjini Dodoma ambao unatarajia kupitisha bajeti ya matumizi na mipango ya maendeleo kwa mwaka 2016/2017.