
Mkuu wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna wa polisi Suleiman Kova.
Akiongea leo Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova ametaka kuwepo kwa udhibiti wa utoaji vibali vya ngoma za usiku maarufu kama vigodoro na kangamoko ambazo amedai kuwa zimekuwa zikichochea uwepo wa genge hilo.
Kwa mujibu wa Kamishna Kova , idadi kubwa ya wahalifu hao wamekamatwa katika maeneo linakopita Bonde la Mto Msimbazi ambako wamekuwa pia wakijihusisha na matukio mengine ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya, unywaji pombe haramu, ubakaji na hata matukio ya ulipizaji kisasi.