Friday , 26th Dec , 2014

Jeshi la polisi limeunda timu ya makachero kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam  wakishirikiana na wa mkoa wa Ruvuma kufanya uchunguzi kuhusiana matukio ya mabomu mkoani humo.

Askari aliyejeruhiwa WP Mariamu Lukindo

Jeshi la polisi limeunda timu ya makachero kutoka makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es salaam  wakishirikiana na wa mkoa wa Ruvuma kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aliyelipukiwa na bomu maeneo ya majengo mjini songea  na kujeruhi askari polisi wawili wakati akijiandaa kuwarushia  askari waliokuwa doria na kisha bomu hilo kumuua mwenyewe.

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Diwani Athumani aliyewasili mjini  Songea kwa helkopta kwa ajili ya tukio hilo ambalo mtu ambaye hajatambulika,   amelipukiwa na bomu na kufariki dunia  wakati akijaribu kuwarushia bomu askari waliokuwa doria na kujeruhi askari wawili PC Mselemu na WP Mariamu Lukindo  ambaye bado amelazwa hospitalini Songea.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said  Mwambungu aliyemtembelea majeruhi Mariamu Lukindo  ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo ni la tatu katika mwaku huu likiwalenga  askari polisi.

Nao wananchi wanaoishi jirani na uliokotokea mlipuko  wa bomu wameeleza hofu waliyokuwa nayo baada ya mlipuko huo wa bomu