Thursday , 24th Jan , 2019

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema atavichunguza vikosi vya usalama baada ya kufanya vitendo vya ukandamizaji wa waandamanaji wiki iliyopita akisema kitendo hicho kinaisaliti Zimbabwe mpya.

Kupitia ukurasa wake, Mnangagwa ameeleza kwamba , ghasia zinazoshuhudiwa na mienendo ya vikosi vya usalama haifai na kwani inahujumu Zimbabwe mpya na kwamba ikibidi hatua zitachukuliwa.

Katika ripoti iliyotolewa imeeleza kwamba watu 12 waliuwawa wiki iliyopita wakati wa maandamano yakupinga ongezeko la bei ya mafuta, huku wengine 74 walijeruhiwa kwa kupigwa risasi

Aidha Tume ya kutetea kutetea haki za binadamu nchini Zimbabwe limewatuhumu maafisa wa usalama kwa kutumia utaratibu wa mateso kutuliza maaandamano.

Ripoti zimeibuka kuwa wanajeshi wanadaiwa kuwapiga na kuwaumiza watu katika maeneo tofauti ya mji mkuu wa Harare.

Akitetea vitendo vilivyofanywa na vikosi vya usalama, Msemaji wa serikali ameiambia BBC kwamba "Mambo yakiharibika wakati mwingine unahitaji kutumia nguvu kiasi."