Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Rais Magufuli atoa maagizo kwa mabalozi wapya

Friday , 20th Jan , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha Mabalozi sita aliowateua jana kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na kuwapa maagizo ya kuitangaza vema na kuiletea maendeleo Tanzania.

Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazil

 

Hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi hao imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza baada ya Mabalozi hao kula viapo vyao, Rais Magufuli amewataka kuiwakilisha vizuri Tanzania katika nchi walizopangiwa kwa kuhakikisha wanasimamia maslahi ya Tanzania.

“Nendeni mkatekeleze kazi zenu kwa upendo mkubwa mkijua umma wa Watanzania upo nyuma yenu, Maslahi ya Watanzania yakawe mbele, Tanzania kwanza ikawe mbele, na mimi nina uhakika mtakuwa mmewafanyia Watanzania mema na mazuri sana”

Rais Magufuli akizungumza na mabalozi baada ya kula viapo

“Ukiona kizuri chochote kwaajili ya Watanzania kilete, mkatetee Tanzania, mkajenge uchumi wa Tanzania, mkaimarishe mahusiano ya Tanzania, mkajenge urafiki wa Watanzania, mkajenge biashara za Watanzania” amesema Rais Magufuli.

Mabalozi walioapishwa ni Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi -Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. James Alex Msekela - Baloziwa Tanzania Geneva - Umoja wa Mataifa, Mhe. Mbelwa Brighton Kairuki - Baloziwa Tanzania nchini China, Mhe. Fatma Mohamed Rajab - Baloziwa Tanzania nchini Qatar, Mhe. George Kahema Madafa - Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mhe. Prof. Elizabeth Kiango Kiondo - Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Rais Magufuli akimuapisha Mhe. Prof. Elizabeth Kiango Kiondo - Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Wakati huo huo, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela amekula kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Baada ya kula kiapo cha Uadilifu, Mhe.Jaji Mstaafu Harold Reginald Nsekela ameongoza kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kwa Mabalozi sita walioapishwa leo kwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine