Wednesday , 24th Jan , 2018

Rais Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahimu Juma kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mh. Robert Kisanga kilichotokea tarehe 23, Januari mwaka huu.

Katika salamu hizo Dkt. Magufuli amesema Jaji Mstaafu Robert Kisanga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa taifa wakati wote wa utumishi wake uliojaa umakini, uchapakazi, uzalendo na ushirikiano na wengine.

Kwa muendelezo wa salamu hizi soma hapa chini