Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ratiba kuagwa wanafunzi wa UDSM kesho

Wednesday , 13th Jun , 2018

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), imetoa taarifa ya kukatisha ratiba ya masomo kwa muda wa masaa matatu kesho Juni 14, 2018 ili kutenga muda wa kuaga miili ya waliokuwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 13, 2018 na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma Profesa Bonaventure Rutinwa na kuongeza kuwa masomo yatasitishwa kuanzia Saa 4:00 asubuhi mpaka 7:00 Mchana.

Taratibu za kuaga miili ya marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Nkrumah uliopo chuoni hapo siku ya kesho Juni 14, 2018 kuanzia Saa 4:00 Asubuhi.

Katika ratiba ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu hao inaonesha, waombolezaji wataanza kuingia katika ukumbi wa Nkrumah kuanzia saa 3:00 asubuhi, na ikifika 3:45 miili ya marehemu hao itaingia ukumbini, ambapo shughuli ya kuaga itaanza rasmi saa 5:40 asubuhi mpaka 6:50 Mchana.

Juni 11, 2018 katika eneo la Riverside-Ubungo wanafunzi wawili na watumishi wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), walifariki Dunia baada ya gari la wagonjwa walilokuwa wamepanda kugoganga na lori la mizigo walipokuwa wanaenda katika Hospitali ya Chuo hicho kwa matibabu.

Waliofariki kutokana na ajali hiyo ni wanafunzi Erasto Sango Steven na Mary Godian Soko na watumishi wawili James Rutayuge ambaye alikuwa ni dereva pamoja na muuguzi msaidizi daraja la pili Jonathan Lung’ando.

 

 

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine