
Mkuu wa mkoa wa Rukwa - Zelothe Stephen
Ameyasema hayo wakati alipomaliza kupanda mti kama ishara ya maadhimisho ya siku ya uhuru yaliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na watumishi wote wa ofisi yake.
Amewataka watumishi wote kila mmoja kuwa na mti wake ambao atauhudumia hadi kukua kwa mti huo, hii ikiwa ni mwanzo wa kampeni ya upandaji miti ili kuokoa Mkoa wa Rukwa kugeuka kuwa jangwa.
Katika kutekeleza Kauli mbiu ya siku ya Uhuru wa Vitendo Mkuu wa Mkoa amezitahadharisha halmashauri hasa idara ya ardhi, elimu, afya na mahakama juu ya kukithiri kwa rushwa.