
Mohamed Dewji
Taarifa iliyotolewa kwa umma kupitia wizara, uamuzi wa kufuta mashamba hayo ni baada ya mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kufutwa mashamba hayo kutokana na kutoendelezwa kwa muda mrefu.
Imeelezwa kuwa mapendekezo yaliwasilishwa kwa Rais John Magufuli kwa nia ya kufutwa mashamba hayo ambayo ni yale yaliyokuwa eneo la Mombo, Mabogo na Kwalukonge wilayani Korogwe.
Akithibitisha uamuzi huo Naibu Waziri wa ardhi Angeline Mabula amesema uamuzi huo wa Rais unalenga kuhakikisha wote waliopewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji wanazingatia masharti na taratibu za uwekezaji.