Sunday , 1st May , 2016

Wataalamu wa Ujenzi nchini Tanzania wameitaka serikali kuwa makini na Makampuni wanayoingia nayo mikataba wa ujenzi wa majengo na barabara nchini kwakuwa baadhi ya wahandisi wanaopewa kufanya kazi hizo hawana viwango.

Wataalamu wa Ujenzi nchini wameitaka serikali kuwa makini na makampuni wanayoingia nayo mkataba wa ujenzi wa majengo na barabara nchini kwakuwa baadhi ya wahandisi wanaopewa kufanya kazi hizo hawana viwango vya kujenga miundombinu kwa tija.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Ujenzi, Mhandisi Jamal Mruma wakati akizungumza na Kurasa na kusema kuwa baadhi ya matatizo yanayosababisha mafuriko ni pamoja na ubunifu mbaya wa miundombinu kosa ambalo linachangiwa na wahandisi ambao wanabuni njia zakupitisha maji chini ya uhitaji wa ukubwa wa eneo.