Monday , 3rd Jun , 2019

Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara amesema miongoni mwa sababu zinazopelekea ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kushuka, ni upingufu wa walimu kwenye baadhi ya shule za msingi hapa nchini.

Sababu nyingine za kushuka kwa matokeo ya wanafunzi wa darasa la saba ni ushiriki hafifu wa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto pindi anapokuwa shuleni na kunakopelekea kutokuwepo kwa ushirikiano baina ya wazazi na walimu.

Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo Bungeni jijini wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge ambapo alikuwa akielezea sababu ya kushuka kwa matokeo ya darasa la 7 kwa wanafunzi waliomaliza 2017.

"Ziko sababu mbalimbali kushuka kwa ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2017, ni upungufu wa walimu, ushiriki wa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto, walimu wa shule ya msingi wanaoajariwa wanaweza kufundisha masomo yote ikiwemo Sanaa na Sayansi pamoja na Hisabati. 2017/18 na 2018/2019 tumeajiri jumla ya walimu 14,422," amesema Waitara.