
pichani mwanaume akimpiga mwanamke.
Akizungumza kwenye kipindi cha MJADALA cha EATV, mwanaharakati wa haki za Wanawake, Faustine Magoti amesema kuwa endapo watekelezaji wa matukio hayo wakifahamu madhara ya ukatili wataacha kutekeleza vitendo hivyo.
"Endapo hata Wizara husika ikiweka mikakati ya kujidhatiti kumaliza vitendo hivyo ikiwemo kushawishi wizara ya Elimu kuandaa mtaala utakaokuwa unafundisha madhara ya ukatili kwa jamii, tutakuwa tumetibu suala hili", amesema Magoti.
Magoti ameongeza kuwa mila na desturi za kiafrika zimechangia kuongeza ukatili, kutokana na wanandoa wengi kukaa kimya pindi wanapotendewa vitendo hivyo kwakuamini kuwa, mengine ni siri za ndani ya nyumba watu wa nje hawapaswi kufahamu.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) asilimia 35 ya wanawake ulimwenguni ni wahanga wa matukio ya ukatili wa kupigwa na kingono.