Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini - Madini, Prof. James Mdoe (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Juliana Pallangyo
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati Madini anaeshughulikia Madini Prof. James Mdoe, ambaye amesema fedha hizo zitawalenga zaidi wachimbaji wadogo ambao ni rasmi na wanatambulika na serikali.
Prof. Mdoe ametumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wadogo ambao bado hawajapata leseni za serikali wajitokeze ili waweze kuingizwa kwenye mfumo rasmi wafaidike na ruzuku hiyo ya serikali kwa ajili ya maendeleo yao.
Prof. Mdoe ameongeza kuwa kutambulika kwa wachimbaji hao wadogo pia kutawasaidia wao pindi wanapokutwa na majanga mbalimbali katika migodi yao ikiwemo kufukiwa katika mashimbo hivyo kupata msaada wa uokozi kwa haraka zaidi.
Amesema kuwa wengi wa wachimbaji hao wadogo ambao hawatambuliki wanafanya shughuli hizo kwa kificho wengi wao wakikwepa kulipa kodi hali innayoipa ugumu serikali kutambua ni wachimbaji wangapi wadogo wanaohitaji msaada wa serikali.