Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serikali yazungumzia ripoti ya uchunguzi wa Lissu

Friday , 14th Sep , 2018

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndio wanachelewesha kukamilika kwa ripoti ya uchunguzi dhidi ya shambulio la mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Waziri Masauni ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali laMbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea bungeni leo Septemba 14, ambalo lilihoji kuwa kumekuwa na matukio mengi ya kihalifu yanatokea ikiwemo kupotea na kutekwa watu, lakini serikali imekuwa ikionesha kuwalinda zaidi watu wao wa karibu na sio wanaharakati wanaoipinga serikali na kuhoji ni lini ripoti ya serikali itakamilika kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Masauni amemtaka Kubenea kufuta kauli yake aliyodai kuwa ni upotoshaji kwa jamii kwani hakuna matabaka katika ulinzi wa raia na mali zao na kusema kuwa “Napenda kujibu swali la Kubenea lakini ningependa kumpinga na kumkosoa vikali kwa kauli yake, kwani hakuna matabaka katika kulinda na kusimamia usalama wa raia na mali zao wote na hakuna matabaka, kuhusu shambulio la Tundu Lissu chama chao hakitoi ushirikiano ikiwemo kumficha dereva ambaye ndiye shuhuda namba moja”.

Aidha Masauni ameongeza kuwa masuala ya kigaidi yanahitaji muda zaidi kukamilisha uchunguzi wake kwakuwa huhusisha taasisi nyingine za nje zaidi ya Jeshi la polisi hivyo unahitaji muda na umakini wa hali ya juu.

Suala la watu wasiojulikana limekuwa likiibua mvutano bungeni kila ifikapo zamu ya kuchangia kwa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuibuka kwa matukio ya utekaji na kupotea kwa watu maarufu kuanzia mwaka 2017 wakiwemo wanahabari na wasanii wa muziki.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine