
Hali ya upatikanaji wa chakula hasa mchele hapa nchini imekuwa ya kuridhisha kwa msimu huu kwani wafanyabiashara wengi wameleta sokoni mchele uliokuwa umehifadhiwa kwa kuhofia kuadimika kwa bidhaa hiyo kabla ya mchele mpya unaotarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu.
Wakiongea na EATV wafanyabiashara hao wamesema ongezeko la mchele sokoni limepelekea bei ya mchele kushuka kutoka shilingi 2500 mpaka shilingi 1600 hivi sasa na kuwafanya watu wengi zaidi kumudu kununua mchele.
Kwa upande mwingine hali hiyo imepelekea baadhi ya wafanyabiashara hasa wale waliokuwa wanahifadhi mchele kwa kusubiri bei ya juu wamejikuta wakuuza kwa bei ya chini kwani bei ya mchele imezidi kushuka na kupelekea wauze bei ya hasara.
Wakati huo huo hali ni tofauti kwa wafanyabiashara wa Maharage kwani upatikanaji wa bidhaa hiyo umekuwa mgumu huku bei ikiwa juu kwa kile wanachodai kuwa ni kupanda kwa bei za pembejeo na mbolea kulikopelekea bidhaa hiyo kuadimika Sokoni.