Thursday , 21st Jul , 2016

Licha ya Shule ya sekondari Kisimiri kuongoza kitaifa katika kufaulishwa wanafunzi wa kidato cha sita bado shule hiyo inakabiliwa na ubovu wa miundombinu pamoja na ukosefu wa uzio wa shule hiyo inayopakana na hifadhi ya taifa ya Arusha.

Afisa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), Rodney Thadeus (kushoto) akimkabidhi bando la sengénge Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Kisimiri, Emmanuel Kisongo.

Mwalimu Mkuu wa Shule Emmanuel Kisongo John hiyo amesema kuwa changamoto inayowakabili ni miundombinu mibovu ikiwemo baadhi ya majengo yanayohitaji ukarabati pamoja na uzio utakaohakikisha hali ya usalama wa wanafunzi.

Amesema kuwa mbali na changomoto hiyo shule hiyo ni moja kati ya shule za kata zilizoongoza kwa matokeo mazuri kitaifa jambo ambalo linawapa faraja ya kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaaluma.

Kwa upande wake Mzazi Halle Jonas na Mwanafunzi wa kidato cha tano Collin Stanley wamesema kuwa matokeo hayo mazuri yamewapa hamasa ya kufanya vizuri katika mitihani yao ili kuweza kufika mbali kielimu na kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla.

Kufuatia changamoto ya ukosefu wa uzio wa shule Kituo cha Mikutano cha AICC kimejitokeza na kutoa msaada wa uzio wa shule hiyo ikiwa ni moja kati ya juhudi za serikali katika elimu.

Shule ya Sekondari Kisimiri imeongoza katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita na kuwa kinara kitaifa jambo ambalo linaifanya shule hiyo kuwa mfano wa kuigwa