
Spika wa Bunge, Job Ndugai
Hayo ameyasema leo, Alhamisi ya Novemba 15 katika mkutano wa 13 kikao cha 8 ambapo miongoni mwa mawaziri hao ni; Dk Agustine Mahiga ambaye hajahudhuria kwa asilimia 35, January Makamba asilimia 37, Profesa Palamagamba Kabudi asilimia 38, William Lukuvi asilimia 41 na Luhaga Mpina asilimia 45.
Pia katika hatua nyingine, Spika Ndugai amewataja wabunge ambao ni watoro zaidi katika vikao na kamati mbalimbali za Bunge.
Amemtaja mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kuwa mbunge mtoro zaidi kuliko wote bungeni na kwenye kamati za Bunge huku Waziri, Jenista Mhagama akiongoza kwa kuwa na mahudhurio bora kuliko wabunge wote bungeni.
“Orodha hii inahusu vikao vyote vya kamati na bunge, unakuta kamati inakaa hakuna waziri wala naibu wake, na wala hakuna taarifa,” amesema Ndugai.