Friday , 1st Apr , 2016

Shirika la Madini nchini (STAMICO),limekutana na wadau wa uendeshaji wa sekta ya uchimbaji mdogo wa madini ili kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Mkurugenzi rasimali watu wa Stamico, Deusdedith Magala,

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Mkurugenzi rasimali watu wa Stamico, Deusdedith Magala, amesema ni kujulishana majukumu ya Stamico, Wizara na wachimbaji wadogo ili kuweka maazimio ya pamoja.

Bw. Magala amesema kila mdau anapaswa kujua majukumu yake katika kuendeleza uchimbaji mdogo kwa kujua pia majukumu ya vyama ya wachimbaji wadogo ili kutoa fursa za kuweza kwa wachimbaji hao wa madini.

Kwa upande wake Makamu wa rais wa shirikisho la Wachimbaji wa madini nchini Dkt. Omary Mzeru, ameiomba Stamico iweke utaratibu mzuri wa kifedha kuwawezesha wachimbaji wadogo ili waweze kujitegemea.

Dkt. Mzeru amesema wachimbaji wadogo changamoto yao kubwa ni kukosa uwezo wa kuendeshea uchimbaji na hakuna utaratibu mzuri wa ulezi kati ya stamico na wachimbaji hao wadogo.

Wadau hao pia wameitaka serikali kuwawezesha kwa kuwapa elimu wachimbaji wadogo ili wapate kupata ruzuku zitakazowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Mkurugenzi rasimali watu wa Stamico, Deusdedith Magala akizungumzia lengo la Mradi