Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Tani 17 za vipodozi zateketezwa Morogoro

Saturday , 21st Jan , 2017

Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kwa kushirikiana na vyombo vya usalama mkoani Morogoro, imeteketeza shehena ya vipodozi vyenye viambata vya sumu huku vingine vikiwa vimekwisha muda wa matumizi yake

Vipodozi hivyo ni kiasi cha tani 17 zenye thamani ya shilingi milioni 57 mali ya mfanyabiashara Agustino Fikiria Tarimo.

Akizungumza mara baada ya kuteketezwa kwa vipodozi hivyo, Mkaguzi wa kanda ya kati kutoka TFDA Sifa Chamgenzi amewasihi wafanyabiashara kuwa waaminifu na kusema mamlaka ya chakula na dawa haitochoka kuwafuatilia wafanyabiashara wote wanaokiuka  sheria za nchi kwa kuuza bidhaa zilizokataliwa kwakuwa zina viambata  vya sumu ambavyo vina madhara makubwa kwa watumiaji.

Zoezi hilo la kukamata vipodozi hivyo lilichukua siku mbili kutokana na mfanyabiashara huyo kuwa na shehena kubwa nyumbani kwake ambapo alifanya nyumba yake kuwa yadi ya kuwekea bidhaa hizo huku ikiwa ni kinyume na taratibu za uhifadhi wa bidhaa hizo.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wananchi mkoani Morogoro, wamesema kuwa, kuteketezwa kwa vipodozi hivyo ni hatua nzuri, kwani asilimia kubwa ya watumiaji ambao ni wanawake wamekuwa wakiharibika ngozi zao, huku wengine  wakipata magonjwa ya ngozi kwa kuwa vipodozi hivyo wanavyotumia kuwa na vimelea vya sumu.

Msikilize hapa Sifa Chamgenzi - Mkaguzi kanda ya kati TFDA

 

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90