Wednesday , 26th Mar , 2014

Tanzania imetajwa kuwa na kiwango cha chini cha wagonjwa wanaougua kifua kikuu chenye usugu wa dawa ambacho hakitibiki na dawa za kawaida zinazotumika kutibu ugonjwa huo.

Mkurugenzi mkuu wa NIMR Dkt Mwele Malecela.

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu NIMR kituo cha Muhimbili Dkt Godfrey Mfinanga, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea hali ya ugonjwa wa kifua kikuu na tafiti mbali mbali zinazofanywa kuhusu ugonjwa huo.

Dkt Mfinanga amesema mbali ya kuwa na idadi ndogo ya wagonjwa wa kifua kikuu sugu, kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo bado kipo juu ambapo kati ya watu laki moja, watu 295 wamebainika kuugua ugonjwa huo.