
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.
Aidha vifaa vyenye thamani ya Sh. bilioni 11.5 vimeanza kuwasili nchini na vimehifadhiwa kwenye maabara za Tume hiyo, ambavyo vimetolewa na Umoja wa Ulaya (EU).
Akiweka jiwe la msingi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema fedha hizo ambazo ni Sh. bilioni 2.3 zimetolewa na serikali zimetokana na fedha za ndani.
"Jengo hili linatarajiwa kukamilika Februari mwaka 2018 na serikali kwa awamu hii ya kwanza imetoa Sh.bilioni 1, fedha nyingine Sh. bilioni 1.3 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa ambayo itaweza kutumiwa na watu mbalimbali nchini na nchi za Afrika. Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha maendeleo ya nchi yasonge mbele haswa katika kuhakikisha tume hii inapata maendeleo na kuchangia fedha katika mfuko huu serikali", alisema Ndalichako.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri alisema maabara hiyo ya kisasa ni moja wapo ya maabara itakayotoa huduma mbalimbali za matumizi salama ya mionzi pamoja na kutoa msaada kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika ngazi ya shahada ya unamilikiwa uzamivu.
Katika maabara hiyo kutakuwa na uhakiki wa vifaa vya kupimia mionzi, chumba cha mionzi mikali kwa ajili ya kupikia vyuma kwa njia ya kupiga picha kwa kutumia mionzi pamoja na chumba cha kutumia mionzi kwa ajili ya shughuli nyingine ambapo kitasimikwa kifaa cha kupima viasili vya mionzi vilivyopo mwilini mwa binadamu.
Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri alisema ujenzi wa maabara hiyo utatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) huku Mhandisi Mshauri wa Mradi ni kampuni ya K$L ARCH forms ya Jijini Dar es Salaam.
"Madini hayo ya urani hapa nchini yamebainika katika maeneo ya Mto Mkuju uliopo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma pamoja na Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma",alisema Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri.
Awali Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Stella Manyanya alitoa rai kwa watumishi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuachana na urasimu kwani Taasisi hiyo ni nyeti na inashughulika na masuala ya mionzi hivyo ni vyema kutoa ushirikiano wa udhibiti wa mionzi hiyo.