Wednesday , 19th Mar , 2014

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imevipongeza vyombo vya habari vya IPP kwa kuwa na mfumo mzuri wa kusimamia utendaji kazi wa shughuli zake za kila siku unaozingatia maadili ya utangazaji.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Bi. Margaret Munyagi wakati walipotembelea vituo vya East Africa Television (EATV), East Africa Radio, ITV/ Radio One pamoja na Capital Television na Capital Radio.

Pamoja na mambo mengine wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA wamevipongeza vituo vya IPP kwa kwenda na wakati kutokana na kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa katika utangazaji ambavyo vimekuwa vikiboresha ubora na kuongeza ufanisi wa kazi.