Saturday , 30th Dec , 2017

Mamlaka ya Mawasiliano nchini  Tanzania  (TCRA), imetangaza kupunguza kiwango cha gharama za mawasiliano ya simu nchini Tanzania kutoka 26.96 kwa dakika moja mwaka huu hadi 15.60 kuanzia 2018.

Akitangaza punguzo hilo la viwango vipya vya mawasiliano ya simu ambavyo vitaanza kutumika Januari  Mosi, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa  TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema viwango hivyo vitaendelea kupungua kila mwaka hadi kufikia shilingi 2 mwaka 2022

Aidha Mhandisi Kilaba amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa matumizi ya simu na kuongeza pato la watoaji huduma wa  mitandao ya simu na taifa kwa ujumla.